UNAWAJUA MASTAA AMBAO WAMEINGIA KENYA KIMYA BILA MTU YOYOTE KUJUA NA KUFANYA YAO KISHA KUSEPA>>Pichaz
Kuna story huwa zinazunguka mitaani kuhusu ishu ya mastaa kuingia Tanzania..
wanatembelea maeneo mbalimbali alafu wanarudi zao kwao !!
Kwenye hizo story kuna za ukweli na nyingine zinatungwa tu mtaani, tuachane na za TZ… nimeipata hii toka Kenya kwa watu +254, nako wako mastaa na watu wakubwa ambao waliwahi kuingia kimyakimya.. pata picha unakutana na Bill Gates mitaa ya Manzese au Kariakoo !! Hiyo ilityokea Kenya aisee..
Kumbe Alicia Keys aliwahi kutua Kenya mwaka 2006 akihamasisha Kampeni za ‘Keep a Child Alive‘ ambazo zinahamasisha kuwajali watoto na familia zilizokumbwa na maambukizi ya HIV.
Nicholas Cage, ni staa wa Movie za action toka Hollywood, jamaa nae aliwahi kufika Kenya kwa ajili ya kushoot vipande vya movie ya ‘Dying of The Light‘.
Bill Gates.. pata picha tajiri namba moja Duniani unakutana nae tu mtaani anakatisha.. Gates aliingia Kenya kimyakimya mwaka 2009 alafu kwenye surprise akakatisha mitaa ya Eldoret.. Wenyeji walishtukia tu baadae kwamba kuna ugeni wa Kimataifa mtaani kwao. Baadae jamaa alitembelea pia mbuga yaMaasai Mara kabla ya kuondoka.
Kocha wa Klabu ya Chelsea, Jose Mourinho nae ni mmoja ya wageni walioingia Kenya kimyakimya mwaka 2010 akatembelea pia mbuga ya Maasai Mara.
Staa wa Mitindo Marekani, Naomi Campell aliwahi pia kuingia bila watu kujua Kenya mwaka huuhuu 2015 kama miezi saba hivi iliyopita.
Mwanamieleka John Cena nae yumo, japo haikuthibitika mpaka sasahivi ila story za mtaani ni kwamba jamaa aliwahi kuingia Kenya kwa ajili ya kushoot Movie yeye na mshkaji wake, Big Show ambaye ni Mcheza Mieleka pia.
No comments