Recent Posts

HAYA HAPA MATOKEO YA LIGI KUU TANZANIA PAMOJA NA PICHA

Mechi za Ligi Kuu soka Tanzania bara ziliendelea kama kawaida kwa michezo kadhaa kupigwa katika viwanja
mbalimbali Tanzania, licha ya kuwa kuna mechi tatu ambazo zimeharishwa kutokana na wachezaji wake wengi kuitwa katika kambi ya timu ya Taifa inayojiandaa na mchezo dhidi ya Malawi, October 3 imepigwa baadhi ya michezo ya Ligi Kuu.
Mechi ambazo zimechezwa Jumamosi ya October 3 katika viwanja mbalimbaliTanzania ni mechi ya Maji Maji FC dhidi ya Mwadui FC katika uwanja wa Maji MajiSongeaMwadui FC ambayo inanolewa na kocha Jamhuri Kiwelu imeibuka na ushindia wa jumla ya goli 1-0 dhidi ya mwenyeji wake Maji Maji FC.
Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika hakuna timu iliyofanikiwa kuona nyavu za mwenzake, dakika ya 56 kipindi cha piliJabir Aziz akaiandikia goli Mwadui FC yaJamhuri Kiwelu, goli ambalo lilidumu katika dakika zote tisini za mchezo na kuifanya Mwadui FC kuondoka na point tatu muhimu dhidi ya Maji Maji FC.
Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu zilizopigwa October 3
Mgambo Shooting 0 – 0 Coastal Union 

No comments