Recent Posts

WACHEZAJI 10 WALIOFANIKIWA KWENYE LIGI KUU ENGLAND

Tangu Ligi Kuu ya England ipewe jina la “English Premier League” mnamo 1992, ilichukuliwa na mashabik
i pamoja na wachambuzi kama ligi bora ya ndani katika ulimwengu wa soka, ya kuvutia wachezaji wengi duniani.
Klabu kama Manchester United, Liverpool, Chelsea na Arsenal walikuwa na mmoja wa wachezaji bora duniani wa kushindana kwa kiwango cha juu katika mashindano ya ndani na Ulaya.
Kutokana na haya, Sokkaa imebainisha wachezaji 10 bora wenye kufanikiwa zaidi katika historia ya Ligi Kuu ya England.
10. Steven Gerrard – Liverpool
Gerrard alikaa muda mrefu akicheza na kuwa nahodha wa Liverpool ambapo alifungwa mabao 186 katika mechi 708.
Licha ya kudumu muda mrefu katika klabu ya Merseyside, Gerrard hakuweza kuinua kombe la Ligi Kuu ya England.
Mataji aliyotwaa katika Liverpool
FA Cup: 2001, 2006.
League Cup: 2001, 2003, 2012.
FA Community Shield: 2006
UEFA Champions League: 2005
UEFA Cup: 2001
UEFA Super Cup: 2001, 2005
9. Frank Lampard - West Ham, Chelsea na Manchester City
Frank Lampard ni mfungaji bora katika Ligi Kuu ya England wa muda wote, alianza amali yake ya soka katika West Ham akafunga mabao 24 katika mechi 148. Alijiunga na Chelsea mnamo 2001 na kufunga mabao 147 katika mechi 429 kabla ajiunge na Manchester City  kwa mkopo ambapo alifunga mabao  mawili katika mechi 32.
Alikuwa na miaka 13 ya mafanikio katika Chelsea, ambapo alishinda mataji kadhaa na kuwa mfungaji bora wa muda wote kwa klabu.
Mataji aliyoshinda katika Chelsea.
FA Premier League (3): 2004–05, 2005–06, 2009–10
FA Cup (4): 2006–07, 2008–09, 2009–10, 2011–12
League Cup (2): 2004–05, 2006–07
FA Community Shield (2): 2005, 2009
UEFA Champions League (1): 2011–12
UEFA Europa League (1): 2012–13
8. Eric Cantona - Leeds United na Manchester United
Cantona alichaguliwa Inside United magazine kama mchezaji bora wa wa daima wa Manchester, alijiunga na upande wa Sir Alex Furguson mnamo mwaka 1992 kutoka Leeds United.
Alishinda mataji manne ya Ligi Kuu ya Uingereza katika kipindi cha miaka mitano akiwa na Manchester United licha ya kupigwa marufuku ya muda mrefu mwaka 1995 kwa kumshambulia shabiki.
Mataji aliyoshinda katika Manchester United
Premier League (4): 1992–93, 1993–94, 1995–96, 1996–97
FA Cup (2): 1993–94, 1995–96
Charity Shield (3): 1993, 1994, 1996
7. Dennis Bergkamp - Arsenal
Bergkamp alikuwa tatizo kubwa kwa mabeki wa Ligi Kuu ya England kutokana na mbinu zake za kudhibiti mpira na atakumbukwa kwa muda mrefu kwa bao alilofunga dhidi ya Newcastle.
Mholanzi huyu alishinda mataji matatu ya Ligi Kuu England na vikombe vinne vya FA katika miaka 11 akiwa Arsenal ambapo alifunga mabao 87 katika mechi 315.
Mataji aliyoshinda katika Arsenal
Premier League (3): 1997–98, 2001–02, 2003–04
FA Cup (4): 1997–98, 2001–02, 2002–03, 2004–05
FA Community Shield (3): 1998, 2002, 2004
6. Patrick Vieira - Arsenal na Manchester City
Mfaransa alitumia muda mrefu wa amali yake ya Ligi Kuu katika Arsenal kutoka 1996 hadi 2005, ambapo alikuwa nahodha pekee wa klabu aliyeshinda taji la ligi bila kushindwa hata mechi moja katika msimu.
Tangu kuondoka kwake kuelekea Juventus mwaka 2005, meneja wa Arsenal Arsene Wenger hajawahi kuwa na nahodha staajabu kama yeye.
Mataji aliyoshinda katika Arsenal na Manchester City
Premier League (3): 1997–98, 2001–02, 2003–04
FA Cup (5): 1997–98, 2001–02, 2002–03, 2004–05, 2010–11
FA Community Shield (4): 1998, 1999, 2002, 2004
5. Cristiano Ronaldo -Manchester United
Mchezaji bora duniani wa sasa alikuwa na miaka 6 ya mafanikio katika Ligi Kuu ya England akiwa Manchester United, ambapo alifunga mabao 84 ya ligi katika mechi 196.
Alishinda mataji matatu mfululizo ya Ligi Kuu vile vile na Ligi ya Mabingwa mwaka 2008 akiwa na Sir Alex Furguson kabla ajiunge na Real Madrid kwa rekodi ya dunia ya ada ya uhamisho ya £80,000,000.
Mataji aliyoshinda katika Manchester United
Premier League: 2006–07, 2007–08, 2008–09
FA Cup: 2003–04
League Cup: 2005–06, 2008–09
FA Community Shield: 2007
UEFA Champions League: 2007–08
FIFA Club World Cup: 2008
4. Paul Scholes - Manchester United
Scholes ni mmoja wa wachezaji wenye mafanikio zaidi katika historia ya soka na alikuwa katika timu ya Manchester United iliyotawala Ligi Kuu ya England katika miaka kadhaa, Mwingereza alishinda jumla ya vikombe 25 vikiwemo 11 vya ligi, na alifunga mabao 155 katika mechi 718 kwa Red Devils.
Mataji aliyoshinda katika Manchester United
Premier League (11): 1995–96, 1996–97, 1998–99, 1999–2000, 2000–01, 2002–03, 2006–07, 2007–08, 2008–09, 2010–11, 2012–13.
FA Cup (3): 1995–96, 1998–99, 2003–04
Football League Cup (2): 2008–09, 2009–10
FA Community Shield (5): 1996, 1997, 2003, 2008, 2010
UEFA Champions League (2):1998–99, 2007–08
Intercontinental Cup (1): 1999
FIFA Club World Cup (1): 2008
3. Alan Shearer - Blackburn Rovers na Newcastle United
Shearer huchukuliwa kama mshambuliaji bora katika historia ya Ligi Kuu ya England; anashikilia rekodi ya kuwa mfungaji bora wa Newcastle na Ligi Kuu ya Uingereza.
Alishinda kombe moja pekee la Ligi Kuu ya Premia akiwa Blackburn Rovers mnamo 1994-1995 alipoandika rekodi ya kufunga mabao 34 katika msimu mmoja.
2. Thierry Henry - Arsenal
Staa wa Ufaransa alicheza miaka nane kwa Arsenal na alionekana kama mmoja wa wachezaji bora zaidi wa kuangalia katika historia ya ligi, ni mfungaji bora wa Arsenal kwa muda wote akiwa na mabao 228 katika mashindano yote.
Katika nyakati zake, Arsenal ilishinda mataji mawili ya ligi na matatu ya Kombe la FA akiwa na Arsenal.
Mataji aliyoshinda katika Arsenal
Premier League (2): 2001–02, 2003–04
FA Cup (3): 2001–02, 2002–03, 2004–05
FA Community Shield (2): 2002, 2004
1. Ryan Giggs - Manchester United
Mchezaji Mwelisi alishinda mataji 13 ya Ligi Kuu ya England na katika amali yake ya soka alicheza kwa klabu moja Manchester United, na hivyo vilimfanya awe mchezaji mwenye mapambo zaidi katika historia ya Ligi Kuu ya England.
Alicheza mechi 960 kwa Manchester United katika mashindano yote kabla astaafu kucheza mpira mwaka 2013.
Mataji aliyotwaa katika Manchester United
Premier League (13): 1992–93, 1993–94, 1995–96, 1996–97, 1998–99, 1999–2000, 2000–01, 2002–03, 2006–07, 2007–08, 2008–09, 2010–11, 2012–13
FA Cup (4): 1993–94, 1995–96, 1998–99, 2003–04
Football League Cup (3): 1991–92, 2005–06, 2008–09
FA Community Shield (9): 1993, 1994, 1996, 1997, 2003, 2007, 2008, 2010, 2013
UEFA Champions League (2): 1998–99, 2007–08
UEFA Super Cup (1): 1991
Intercontinental Cup (1): 1999
FIFA Club World Cup (1): 2008

No comments