Recent Posts

PICHA ZA RONALDO AKIWA KWENYE NDEGE BINAFSI AKIENDA KUJIUNGA NA TIMU YA TAIFA

Ikiwa ni mapumziko mafupi ya Ligi Kuu mbalimbali duniani ili kupisha michezo kadha ya timu za taifa
iliyo katika kalenda za FIFAReal Madrid ya Hispania ilimaliza mechi yake ya weekend kabla ya kwenda mapumziko mafupi dhidi ya Atletico Madrid na mechi kumalizika kwa sare ya goli 1-1, mshambuliaji wao Cristiano Ronaldo amekodi ndege binafsi kwenda kujiunga na timu yake ya taifa.
Cristiano Ronaldo ambaye alikuwa anahitaji goli moja tu ili avunje rekodi ya ufungaji wa muda wote wa klabu ya Real Madrid iliyokuwa inashikiliwa na Raul, amesafiri na ndege binafsi kuelekea kujiunga na kambi ya timu ya taifa yaUreno, ambayo itacheza mechi mbili za kuwania kufuzu michuano ya mataifa yaUlaya.
Licha ya Cristiano Ronaldo kutofanikisha lengo lake la kuwa mfungaji bora wa muda wote wa klabu ya Real Madrid, tayari ndio mchezaji wa timu ya taifa yaUreno ambaye ndio mfungaji bora wa muda wote wa nchi hiyo, Cristiano Ronaldo ana jumla ya goli 55 alizofunga akiwa na timu yake y taifa. Lakini anatajwa kufunga zaidi ya magoli 500 ikiwa ni jumla ya goli alizofunga katika vilabu alivyochezea na timu ya taifa.

No comments