Recent Posts

HAYA HAPA MANENO YA MOURINHO BAADA YA CHELSEA KUENDELEA KUPOKEA KIPIGO

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amesema hana mpango wa
kuihama klabu yake pamoja na kuwa katika kipindi kigumu zaidi hivi sasa. Lakini Mourinho akasema, “kama klabu itataka kuniondoa basi nifukuzeni wenyewe, mimi sikimbii majukumu yangu”.
Akiongea mara baada ya kupokea kichapo cha magoli 3-1 mbele ya Southampton katika uwanja wa Stamford Bridge, Mourinho ameiambia Sky Sports kwamba hawezi kukimbia majukumu yake kwani anaamini timu take itamaliza ligi ndani ya nafasi nne za juu (top four).
Mourinho anaongeza, “nataka niweke sawa kwanza, sikimbii majukumu yangu..”
“Mbili, kama klabu inataka kunifukuza, basi ifanye hivyo kwakua mimi sifikirii kuondoka”.
“Tatu, kama wakinifukuza, litakua ni jambo kubwa kufanyika katika historia ya klabu kwani watakua wamemfukuza kocha bora zaidi duniani”.
Chelsea inashika nafasi ya 16 hivi sasa baada ya kupoteza michezo minne, kushinda miwili na sare miwili.
Mourinho anasema ubingwa hautakua rahisi hivi sasa kwake kwakua kuna gepu kubwa sana kati ya Chelsea na vinara wa ligi lakini akasema hata iweje watamaliza ndani ya top four.
Wakati huo huo Mourinho amewatupia lawama waamuzi kwa madai wanaogopa kuipa maamuzi Chelsea kwa kuhofia kukosolewa na wachambuzi wa mpira nchini England.

No comments