Recent Posts

SIR ALEX FERGUSON ARUDI UPYA NDANI YA OLD TRAFFORD KUFUNDISHA

Ferguson atamfundisha tena Beckham akiwa ndani ya Old trafford tena mwezi ujao
.
Sir Alex Ferguson atamfundisha tena Beckam wakati wakicheza  mechi kwa ajili ya kuchangia mfuko wa UNICEF mechi itakayo chezwa old trafford.
Beckham atakuwa nahodha wa kikosi kitachoundwa na wachezaji waliwahi kuwika uingireza wakati watakapo cheza dhidi ya wacheza waliowahi kuwika duniani wakiongozwa na mchezaji wa zamani wa Real madrid Zinedine Zidane. Mchezo huo utachezwa siku ya Jumamosi tarehe 14 November.
Carlo Ancelotti, mmoja wa makocha waliokuwa wakitarajiwa kuchukua nafasi ya sir Ferguson ndani ya manchester utd atakuwa akiifundisha timu pinzani kwenye mechi hiyo ya kukusanya fedha kwa ajili ya watoto kwa kupitia mauzo ya tiketi katika mchezo huo. Fedha zitakazopatikana zitakwenda kusaidia watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu.
Beckham amesema;" Nataka dunia iwe sehemu salama kwa watoto kuishi na kuepukana na majanga, umasikini na walindwe kupata magonjwa. Hii mechi inanipa nafasi ya kukusanya fedha ambazo zitaweza kuwasaidia watoto hawa wanaohitaji msaada huu sana"

No comments