Pluijm aelezea sababu za Azam kusawazisha
Hans van der Pluijm, kocha mkuu wa timu ya Yanga
Kocha mkuu wa Yanga Hans van Pluijm amesema mchezo kati ya Yanga dhidi ya Azam ulikuwa mzuri licha ya timu yake kushindwa kuibuka na ushindi baada ya Azam kutoka nyuma na kusawazisha goli zikiwa zimebaki dakika chache mchezo kumalizika.
“Nilitarajia mechi kuwa ngumu kama ilivyokuwa, Azam walicheza kwa kutumia nguvu kuliko sisi na hilo ndio tatizo lililotukaili. Kama unapata penati dakika za mwisho na ukashindwa kufunga ni tatizo pia”, alisema Hans.
“Goli tulilofunga dhidi ya Azam lilikuwa ni goli zuri, lakini goli tulilofungwa na Azam lilitokana na makosa ya ukabaji wa mabeki, tunatakiwa kuwa makini dakika zote za mchezo”.
Kipre Tchetche aliifungia Azam goli la kusawazisha zikiwa zimesalia dakika tisa ili mchezo kumalizika baada ya Yanga kufunga goli lao kupitia kwa Donald Ngoma dakika ya 45 kipindi cha kwanza.
No comments