Recent Posts

Stewart Hall aishushia kombora zito Tff

Stewart John Hall, kocha mkuu wa Azam FC 

Baada ya mchezo kati ya Yanga dhidi ya Azam uliomalizika kwa sare ya kufungana goli 1-1, hali ilikuwa tofauti ilipofika zamu ya kocha wa Azam FC Stewart Hall kugoma kuongea juu ya mchezo wenyewe na badala yake akashusha ‘rungu’ la lawama kwa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF).

Stewart ambaye jana hakukaa kwenye benchi la ufundi kuiongoza timu yake kutokana na kutumikia adhabu, alikaa jukwaani huku akiishuhudia timu yake aikitoka nyuma kwa goli moja na baadae kusawazisha goli hilo na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa sare.

“Habari za hizi, hadi TFF itakapo zuia suala la rushwa kwa waamuzi wa soka la Tanzania ndipo mambo yatakwenda sawa vinginevyo hakutakuwa na ligi, usiku mwema”, aliaga kocha huyo aliyeonekana kuchukizwa na maamuzi ya jana wakati timu yake ikicheza dhidi ya Yanga.

Mara baada ya kusema hayo, Stewart linyanyuka kwenye kiti na kuondoka kwa hasira kutoka kwenye chumba cha habari na kuelekea nje.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi Abdallah Kambuzi kutoka Shinyanga, wachezaji wa Azam walimzonga mwamuzi huyo baada ya kuamua ipigwe penati kwenye lango la Azam baada ya golikipa wa Azam Aishi Manula kumwangusha Simon Msuva kwenye eneo la hatari.

No comments