Recent Posts

NEYMAR AINGIA MATATIZONI NA SERIKALI YA BRAZIL AMBAPO KWA SASA GARI YAKE IMEKAMATWA


Staa wa Soka, mkali mwingine toka Brazil ambaye anachezea Klabu ya Barcelonahii sio taarifa nzuri kwake, wafatiliaji
wa mambo wanasema inafanana kabisa na ishu ambayo aliwahi kuhusishwa nayo pia ya kukwepa kulipa Kodi ya Serikali mwaka 2013 alipokuwa anahama kutoka Klabu ya Santos kwenda Barcelona.
Kingine kinachomhusu Neymar nyumbani kwao Brazil ni kwamba, Idara ya Serikali ya Brazil inayohusika na ukusanyaji wa Mapato imelikamata gari lake aina yaPorsche na kesi inayohusu gari hilo ni kwamba inadaiwa Neymar alikiuka Sheria wakati anaanza kulimiliki gari hilo, na mpaka hatua za mwisho wakati gari linaingizwa Brazil na linatua mikononi mwa Neymar mwenyewe kuna kanuni za masuala ya mapato zilikiukwa !!
Taarifa zilizogusa Vyombo vya Habari kuhusu ishu hiyo zinasema Neymar na baba yake walishinda gari hilo kwenye mchezo wa bahati nasibu baada yaNeymar kuwa mfungaji Mwaka bora Mwaka 2011 kwenye Michuano ya Vijana wenye umri chini ya miaka 20.
Mpaka sasahivi gari linashikiliwa na Serikali na wamesema halitoachiwa mpaka Kesi yake na watu wa Mamlaka ya Mapato iishe… Hii inakuwa mara ya pili kwa Neymar kuhusishwa na ishu ya kukwepa kulipa Kodi nyumbani kwao Brazil.

No comments