Recent Posts

HUYU HAPA NDIYE MCHEZAJI WA EPL PEKEE AMBAE ANAWEZA KUCHEZA REAL MADRID, BUYERN NA BARCA

Kutokana na kile kinachoendelea hivi sasa kuhusiana na kuboronga kwa timu za England katika michuano ya klabu bingwa Ulaya, kiungo legendari wa Manchester Un
ited Paul Scholes amesema labda Sergio Aguero ndiye anaweza kupata namba katika vikosi vya Madrid na Bayern Munich.
Akiongea wakati wa uchambuzi wa michuano ya vilabu bingwa Ulaya kupitia BT Sport, Scholes alisema ligi kuu England hivi sasa haina wachezaji wenye ubora wa dunia kama ilivyo kwa mataifa kama Spain na Ujerumani.
Scholes anasema wachezaji bora wote hivi sasa wanapatikana Madrid, Bayern Munich na Barcelona pekee huku akisema Juventus na PSG wanafuatia kwa karibu.
Alipoulizwa kama kuna mchezaji anayecheza ligi kuu nchini England anaweza kupata namba katika vikosi vya Real Madrid, Barcelona na Bayern Munich, Scholes anasema, “hakuna. Labda Aguero ndiye ana vitu vya tofauti.”
Mjadala ni mkubwa hivi sasa nchini England kutokana na kuporomoka kwa viwango vya ubora wa vilabu katika michuano ya ulaya na kufanya ufalme ule wa zamani kuhamia Hispania na Ujerumani.

No comments