JEZI YA BUSUNGU MCHEZAJI WA YANGA YAGOMBANIWA MOROGORO
Licha
ya matokeo ya ushindi wa Yanga wa magoli 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar
magoli yaliyofungwa na Malimi Busungu pamoja na Donald Ngoma na kuvunja
mwiko wa kutopata ushindi kwa muda mrefu katika uwanja wa Jamhuri, kuna
matukio mengine yalito
kea Morogoro ambayo yalivutia wengi.
Kivutio kikubwa kwenye mchezo huo
walikuwa ni mashabiki wa Yanga ambao walikuwa wakisema wamekwenda
uwanjani kumshuhudia Malimi Busungu, Amis Tambwe na Thabani Kamusoko.
Lakini hata wafanya biashara wa
jezi ambao hukaa nje ya uwanja pindi ambapo Simba au Yanga zinapokuwa
zinacheza, nao wamesema kwamba jezi ambazo zilikuwa zikiuzika jana
kwenye mchezo kati ya Yanga na Mtibwa ilikuwa ni ya Malimi Busungu
ikifuatiwa na Amis Tambwe pamoja na Thaban Kamusoko.
Hata hivyo bado rekodi ya uuzwaji
wa jezi ya Jaja iliyowekwa msimu uliopita haikufikiwa, kitu ambacho
vilabu vya Tanzania vinatakiwa kujifunza ni kwamba, mbali na kusajili
wachezaji ambao wataisaidia timu ndani ya dakika 90, wananafasi kubwa ya
kuisaidia timu kuingiza mapato kutokana na kuuza jezi na bidhaa
nyingine za klabu kama klabu hizo zitaweka taratibu sahihi.
Simba wamejitahidi kuzindua jezi
zao mpya ambazo wanaziuza kwa utaratibu lakini wafanya biashara wengi wa
jezi mjini Morogoro jana walionekana wanauza jezi za Simba zamani.
Walipoulizwa kwanini wanauza jezi
za zamani wakati tayari klabu hiyo inajezi mpya inazozitumia kwenye
msimu huu walisema kwamba, bado klabu hiyo haijaweka utaratibu wa uuzaji
wa jezi hizo mpya kwasababu upatikanaji wa faida unakuwa mgumu kwao
No comments