Recent Posts

HAWA HAPA WALIONGIA WAPYA KIKOSI CHA ENGLAND NA WALIOTEMWA



Kocha wa timu ya taifa Roy Hodgson amewajumuisha kiungo wa tottenham Dele Alli na mshambuliaji wa Liverpool Dany Ings kwenye kikosi chake kwa mara ya kwanza kwa ajili ya kupambana na Estonia na Lithunia kwenye michuona ya kufuzu euro 2016.

Alli ambae anapata nafasi kikosi cha kwanza kwenye klabu yake ya spurs kwenye msimu huu, alijiunga na spurs akitokea kwenye club ya MK Dons inayoshiriki championship.
Alli ambae ana miaka 19 aliifungia spurs goli la kwanza walipotoka draw na timu ya leicester city mwezi wa nane.
Hodgson amesema " Tumekuwa tukivutiwa nae mda mrefu na sasa ndio mda wa kumjua vizuri zaidi"
Hodgson pia amesema " Tunafikiri ni bora Daniel Sturridge kuongeza nguvu na kujiweka vizuri kwa ajili ya msimu huu liverpool tunataini kumuona akiwa vizuri mwezi ujao"
Sturridge nae hajaitwa kwenye kikosi hicho cha england.

No comments