Recent Posts

Mwambusi atoboa siri ya kuhamia Yanga

Juma Mwambusi, kocha wa zamani wa Mbeya City aliyejiunga na kikosi cha Yanga kuziba nafasi ya Charles Boniface Mkwasa aliyepewa mkataba wa kudumu kuifundisha timu ya taifa

Yanga tayari wameshampa mkataba wa mwaka mmoja na nusu aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya Mbeya City Juma Mwambusi kwa ajili ya kuziba nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa kocha msaidizi wa timu hiyo Charles Boniface Mkwasa ambaye kwasasa ni kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.

Shafiidauda amefanya mahojiano na Mwambusi kutaka kujua kwa nini ameamua kujiunga na kikosi cha Yanga na kuwa kocha msaidizi wakati alikuwa ni kocha mkuu wa timu ya Mbeya City ambayo alidumu nayo kwa takribani miaka mitano.

Shaffihdauda: Mchakato wa wewe kwenda Yanga ulikuwaje?

Mwambui: Kikubwa ni wao wamependezwa na kazi yangu wakaniomba kuja kuwasaidia sidhani kama kuna kingine, tumekubaliana na kuafikiana kufanya kazi pamoja.

Shaffihdauda: Wewe ni miongoni mwa waasisi wa Mbeya City tangu haijaanza kucheza ligi kuu, walipokeaje taarifa za wewe kuondoka kwenye klabu ya Mbeya City?

Mwambusi: Kila mtu kwa upande wake alikuwa na majonzi lakini kazi kuna mambo mengine inabidi yafanyike ili maisha yazidi kuendelea na ni changamoto mpya wao wanajua nimekaa nao kwa siku nyingi kwasababu nilitaka niandike historia kwenye timu moja.

Maana kuna watu wanasema mwalimu amekaa sana inawezekana kuna undugu unatumika lakini mimi naona wanakosa weledi kwasababu ukiangalia Sir Alex Ferguson hakuwa na undugu ndani ya Manchester lakini alikaa kwa muda mrefu. Mimi nilitaka nikae hata kwa miaka 10 hadi 12 ndani ya Mbeya City lakini imetokea nafasi ya kuondoka inabidi iwe hivyo japo na mimi naikitika.

Shaffihdaudua: Umeondoka Mbeya City ukiwa kama kocha mkuu, umeenda Yanga kuwa kocha msaidizi kipi kimekusukuma kuachia nafasi ya ukocha mkuu na kwenda kuwa kocha msaidizi?

Mwambusi: Yanga ni timu kubwa na kongwe na inamipango mizuri na mipango yao ndio imenivutia mimi hasa kushiriki michuano ya kimataifa kwasababu mashindano ya Afrika wanashiriki kama mabingwa wa Tanzania. Nimeshaipeleka Mbeya City kimatifa mara moja tangu tumepanda ligi lakini bado nahitaji changamoto nyingine ndiomaana nimekubali kujiunga nao.

Shaffihdauda: Ulikuwa mwajiriwa wa halimashauri ya jiji la Mbeya kabla ya Mbeya City haijaanzishwa au uliajiriwa kama kocha tu?

Mwambusi: Sijawahi kuwa mwajiriwa wa jiji, mimi ni mfanyakazi kama mwalimu wa mpira lakini sikuwa mwajiriwa kama viongongozi wengine kama katibu wa timu na wengine.

Shaffihdauda: Mashabiki wa Mbeya City wamekuwa wakiisapoti sana timu yao na mara nyingi umekuwa ukiwashukuru kwa kile wanachokifanya, unawaambia nini wakati huu utakapokuwa nje ya timu yao?

Mwambusi: Bado tunatakiwa tuijenge timu, mpira ndivyo ulivyo kwasababu mimi kama familia ya Mbeya City nikiwa na daktari pamoja na Kit Manager na baadhi ya viongozi wa timu ndio waasisi wa timu mpaka imekuja kupanda daraja. Kwahiyo mimi ni mmoja wa waasisi wa ile timu na wao wanajua hilo. Nawaambia mimi bado ni wao, wnatakiwa kusonga mbele na kuiombea Mbeya City iweze kuinuka kupata matokeo mazuri.

Shaffihdauda: Maranyingi makocha ambao wamekaa muda mrefu na timu pindi wanapoondoka kwa amani hupewa nafasi ya kupendekeza warithi wao, vipi kwa upande wako umehusishwa kupendekeza kocha atakaerithi majukumu yako?

Mwambusi: Mwalimu aliyebaki pale ni mwalimu mwenye leseni ‘A’ kama mimi na ameshafundisha timu za ligi kuu, kwahiyo kitu kikubwa ni kumpa ushirikiano ambao walikuwa wananipa mimi. Benchi la ufundi halijaharibika sana kwasababu wale waliokuwepo wakati nipo mimi ndio wapo sasahivi kwahiyo wampe ushirikiano na akitaka ushauri wangu nitampa.

No comments