Recent Posts

Maneno ya Thomas Muller kuhusu kuhamia Manchester united

Ni takribani wiki moja baada ya CEO wa klabu ya FC Bayern Munich kuzungumza kwamba Manchester United waache kumtumia barua pepe juu ya usajili wa kiungo/mshambuliaji Thomas Muller, sasa mchezaji huo mwenyewe amezungumza.
  Muller ambaye amekuwa akihusishwa na Manchester United kwa muda mrefu amezungumzia kuhusu kuhamia kwenye ligi kuu ya England na kukiri mishahara inayolipwa kwenye ligi hiyo inashawishi sana.

Muller, akizungumza gazeti la Ujerumani la Welt am Sonntag, alisema: ‘Mwishoni kabisa, tusisahau kwamba kucheza soka ndio kazi yetu.

‘Hivyo watu lazima wakubali mishahara inachangia sana katika kufanya maamuzi ya mwanasoka. Kiukweli mishahara inayolipwa katika Premier League inashawishi sana. Utakuwa ni unafki kukataa hilo.

‘Inabidi uangalie package yote wanayotoa ili kujua kama inakufaa. Kilicho bora kwako kwa siku moja sio lazima kiwe kizuri siku moja baadae.

‘Najua vilabu vingi vya Ujerumani havipendezwi na matumizi ya vilabu vya EPL, lakini mwisho wa siku nadhani hili ni jambo zuri kwa kila mtu.
‘Ni jambo zuri kwa kila klabu kuwekeza fedha nyingi.’

  Kauli hizi za Muller zitampa moyo Louis van Gaal katika jaribio lake kumleta mjerumani huyo Old Trafford kutoka Bayern Munich.

No comments