Recent Posts

DROGBA AZIDI KUTUPIA HUKO MAREKANI MECHI TISA GOLI TISA



Mshambuliaji Didier Drogba amefunga bonge la bao, umbali wa mita 30 hivi wakati akiitumikia timu yake ya Montreal katika Ligi Kuu Marekani maarufu kama MLS.
Bao hilo linakuwa ni la tisa kwake katika mechi tisa za Major League alizocheza.

Bao hilo la Drogba limeizaidia timu yake kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Orlando City.
Kwa sasa Montreal imeamsha matumaini ya kumaliza vizuri hatua hiyo ya mtoano katika ligi.
Tayari ina pointi 45 kwa upande wa msimamo wa ligi.
Drogba aliyefanya vizuri akiwa na Chelsea  nchini England, amekuwa akifanya vema nchini Marekani.

No comments