Recent Posts

MBWANA SAMATA AZIDI KUNG'AA NI BAADA YA TP MAZEMBE KUICHAKAZA AL MERREICK YA SUDANI NA KUTINGA FAINALI YA MICHUANO KLABU BINGWA AFRIKA

Klabu ya Demokrasia ya Congo TP Mazembe imetinga kwenye fainali za mwaka huu za kombe la
Klabu bingwa Afrika baada ya kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Al-Merreikh ya Sudan katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja Stade TP Mazembe jijini Lubumbashi.
TP Mazembe imeingia fainali Kwa ushindi wa jumla ya mabao 4-2 baada ya kupoteza mchezo wao wakwanza dhidi ya Al-Merreikh Kwa mabao 2-1.
Baada ya mchezo huu kuwa sare ya bila kufungana kwenye kipindi cha kwanza, Mbwana Samatta alifunga bao la kwanza la mchezo kwenye dakika ya 52.
Mazembe ambao hawaja poteza mchezo wowote wa nyumbani walifanya mabadiliko ya kuongeza nguvu kwenye safu ya mashambulizi dakika ya 57 na ilimuona Mshambuliaji mtanzania Thomas Ulimwengu akichukua nafasi ya Rainford Kalaba.
Samatta aliendelea kuonyesha makali yake baada ya kujipatia goli lake la pili dakika ya 69 kabla ya mshambuliaji Rodger Assalé kufanga bao la tatu dakika ya 70.
Mabao haya mawili yanamuweka Samatta katika nafasi nzuri kwenye safu wa wafungaji bora akiwa na magoli 6 chini ya mshambuliaji wa Al-Merreikh Bakri Al-Madina ambae amefunga mabao 7 licha ya timu yake kuaga mashindano Leo.
TP Mazembe itakutana na USM Alger ya Algeria kwenye fainali ambayo wataanzia kucheza ugenini kati ya tarehe 30 Oktoba na tarehe 1 Novemba, huku Mechi ya mzunguko wapili kuchezwa kati ya tarehe 6 na tarehe 8 Novemba jijini Lubumbashi.

No comments