Recent Posts

MATOKEO YA MECHI YA TAIFA STARS VS MALAWI (+PICHAZ)

October 7 ni siku ambayo timu ya taifa yaTanzania Taifa Stars ilishuka dimbani kucheza mechi ya hatua z
a awali za kuwania kufuzu kucheza michuano ya Kombe la Dunia 2018. Huu ulikuwa ni ufunguzi rasmi wa kuanza kwa hatua za awali za mechi hizo. Taifa Starsinayofundishwa na Charles Boniface Mkwasa ilianza kampeni yake kwa kucheza na timu ya taifa ya Malawi.
Kikosi cha Taifa Stars
Taifa Stars ambayo ilikuwa na nyota wake wote hadi wanaocheza soka la kulipwa katika nchi za Afrika Kusini naCongo, imeingia ikiwa na rekodi ya kufanya vizuri katika mechi yake ya mwisho dhidi ya Nigeria kwa kutoka bila kufungana na mabingwa hao wa zamani wa Kombe la mataifa ya AfrikaTaifa Stars katika Viwango vya FIFA ipo nafasi ya 136 wakati Malawi wakiwa nafasi ya 101.
Kikosi cha Malawi
Mechi hiyo iliyochezwa katika dimba la Uwanja wa Taifa Dar Es Salaamimemalizika kwa timu ya taifa yaTanzania kuibuka na ushindi wa jumla ya goli 2-0, magoli ya Taifa Stars yalifungwa na Mbwana Samatta dakika 19 naThomas Ulimwengu dakika ya 22 . Taifa Stars itacheza mechi ya marudiano na timu ya taifa ya Malawi Jumapili ya October 11 mjini Blantyre Malawi.
Mrisho Ngassa akiwania mpira na Limbikani Mzava
Mbwana Samatta akishangilia goli lake akiwa na Thomas Ulimwengu
Thomas Ulimwengu katika harakati za kutafuta goli
Mashabiki wa Taifa Stars
Shomari Kapombe akijaribu kumpita beki wa Malawi
Thomas Ulimwengu akiwa chini akiugulia maumivu
Thomas Ulimwengu akishangilia goli na Mbwana Samatta baada ya kufunga goli la pili
Manahodha wa timu zote mbili Nadir na Mzava wakiwa na waamuzi
Mashabiki wa Stars akiwa kavaa kinyago
Samatta na Mzava wakiwania mpira
Thomas Ulimwengu akipiga krosi wakati ambao Mivale Gabeya akijaribu kuzuia
Kocha wa Yanga Hans van Pluijm ni mmoja kati ya waliohudhduria mchezo huo

No comments