Recent Posts

Martial amzidi uwezo Ronaldo

Baada ya jana usiku kufunga goli dhidi ya CSKA Moscow ya Urusi katika michuano ya klabu bingwa Ulaya, kijana Anthony Martial ameweka rekodi ambayo ilimshinda Cristiano Rinaldo akiwa Old Trafford.

Katika umri wa miaka 19 Martial ameshafunga magoli 5 katika mechi 9, huku katika umri huo huo ilimchukua Cristiano Ronaldo mechi 39 kufunga magoli hayo 5.

Kijana Huyo raia wa Ufaransa amekua na mwanzo mzuri huku akimudu presha iliyopo Old Trafford sanjari na dau kubwa sana alilosajiliwa akitokea Monaco ya Ufaransa.

Anthony Martial alitua Old Trafford akiwa hafahamiki hadi na nahodha wa klabu hiyo Wayne Rooney, lakini hadi sasa amekua miongoni mwa wachezaji tegemezi klabuni akiwapiku hata akina Memphis Depay ambao wana majina makubwa zaidi yake.

No comments