Recent Posts

Usajili wa kwanza wa Jurgen Klop liverpool huu hapa

Kocha mpya wa Liverpool Jurgen Klopp anatazamia kumrudisha kikosini winga Lazor Markovic anayekipiga Fernabache kwa mkopo ifikapo January mwakani.

Winga Hugo mwenye miaka 21 alinunuliwa kwa pauni milioni 20 akitokea Benfica ya Ureno na kocha Brendan Rodgers msimu uliopita lakini alishindwa kutamba na hata kuruhusiwa kwenda kuongeza uwezo nchini Uturuki.

Markovic amekua katika kiwango kizuri hivi sasa na Fernabahce kabla ya kupata maumivu ya mgongo hivi karibuni.

Klopp ambaye anakabiliwa na majeruhi lukuki katika kikosi chake hivi sasa, anafikiria kumrudisha tena Markovic endapo tu klabu anayoichezea sasa kwa mkopo itaridhia kutokana na kuwa na mkataba naye wa mkopo wa msimu mzima.

Fernabahce wanamlipa mshahara wote kijana huyo lakini hawana ruhusa ya kumsajili moja kwa moja kijana huyo mwenye miaka 21

No comments