Recent Posts

KOCHA WA MALAWI - TUMEKUJA TANZANIA KWA SHUGHULI MAALUM

Kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Malawi Nsanzurwimo Ramadhan
amesema kikosi chake cha Malawi kimekuja Tanzania kwa shughuli maalum.
Kocha huyo raia wa Burundi aliyeteuliwa hivi karibuni kama msaidizi wa kocha mkuu Ernest Mtawali amesisitiza kwamba wachezaji wake wote wako vizuri kasoro mmoja aliyebaki Afrika kusini.
“Tupo tayari na wachezaji wote wapo vizuri, tumepoteza mchezaji mmoja kutoka Afrika kusini ambaye alikua na mechi jumapili kwa hakufika,”

Kocha huyo ameongezea kusema kwa kujiamini kuwa hawakuja Tanzania kwa ajili ya kutalii.
“Hatukuja Tanzania kwa matembezi, tumekuja kishughuli.” aliongea kwa kusisitiza
“Tumekuja na vijana chipukizi na hatutazamii matokeo ya leo, bali matokeo ya kesho. Nategemea mchezo huo wa kesho utakuwa mzuri sana.”

Taifa stars watacheza dhidi ya Malawi katika uwanja wa Taifa siku ya Jumatano kwenye majira ya saa kumi za jioni.

No comments