Recent Posts

Fabio Capello: Akili ya Mourinho imechoka

Kocha wa zamani Uingereza Fabio Capello
Fabio Capello ametuma shambulizi la ajabu kwa Jose Mourinho, akidai
wachezaji wa Chelsea wamechoka kiakili baada ya kufanya kazi na Special One.
Mabingwa wa Ligi Kuu wamekuwa na mwanzo mbaya msimu huu, wachezaji, binafsi, wameshakata tamaa ya kutetea ubingwa wao.
Mourinho alipewa kura ya imani kutoka kwa watu na bodi ya Blues jana – ikiwa ni hatua ya ajabu chini ya mmliki Roman Abramovich.
Jose Mourinho a.k.a Special One
Na kocha wa zamani wa Uingereza Capello hajashangazwa na matatizo ya Chelsea, akidai kuwa Mreno huyo amechoka kiakili na kikosi chake.
“Mourinho ni mtu wa mikakati. Ana wakati mgumu, ameiomba klabu iwe nawe au ipingane naye,” alisema Muitalia.
“Mourinho ni kocha mzuri, ila baada ya mwaka na nusu, wachezaji wamechoka,  wachezaji wake hawawezi kumpa anachotaka.”

No comments