Recent Posts

Facebook kuzindua satellite ya intaneti Afrika

Mark Zuckerberg amesema satellite hiyo itaanza kufanya kazi katikati ya 2016

Facebook kuzindua satellite ambayo itatoa huduma ya intaneti katika maeneo ya ndani Afrika, muasisi wa mtandao wa kijamii Mark Zuckerberg ametangaza.
Wakiwa katika ushirikiano na watoa huduma wa Ufaransa Eutelsat, Facebook inatumaini satellite ya kwanza itazinduliwa 2016.
“Tunaendelea kufanya kazi kuunganisha ulimwengu mzima – hata kama inamaanisha kuzindi sayari yetu,” Mark Zuckerberg alieleza kwenye mtandao wa Facebook.
Muasisi wa Facebook Mark Zuckerberg
Mradi huo ni sehemu ya mradi wa Intaneti ya Facebook.org, ambao umekosolewa katika baadhi ya mataifa.
Katika baadhi ya maeneo, hususani India, biashara zilikasirikia mipango iliyopewa Facebook, na washirika wake, kuwa haikuwa na faida katika soko la intaneti linaloendelea.
Internet.org inapitia njia tofauti za kutoa intaneti kwenye maeneo magumu kufika

No comments