Recent Posts

Hazard kuondoka mwishoni mwa msimu huu kuelekea timu hii


L’Equipe gazeti la nchini Hispania limeandika habari ambayo sio nzuri kwa mashabiki wa timu ya Chelsea likiandika Eden Hazard kaamua kuondoka chelsea mwisho wa msimu huu na kuelekea real madrid.

Habari hizi zimekuja wiki moja baada ya mshambiliaji huyo wa Ubelgiji kuongelewa sana kuhusu kuhamia Madrid baada ya kutopangwa kwenye mechi dhidi ya Astoni Villa mchezo wa ligi kuu ya Uingereza.

Hata hivyo Hazard amecheza mechi ya klabu bingwa Ulaya dhidi ya Dynamo Kiev usiku wa jummanne kwenye klabu bingwa Ulaya inaonekana kama vile hakuna tena tatizo.

L’Equipe limereprt kuwa Hazard amechoshwa na maisha ya London na ligi ya Uingereza na tayari ameshaiyambia familia yake, rafiki zake pamoja na baadhi ya raia wenzake wa ubelgiji kuwa anataka kuhama klabuni hapo.

Copy ya gazeti hilo hii hapo chini.

No comments