Recent Posts

Breaking News:Samatta atajwa katika kinyanganyiro cha mchezaji bora Afrika

CAF imetoa majina ya Tuzo mbili ile ya Mwanasoka Bora wa Mwaka Afrika na Mwanasoka Bora wa Mwaka Anayecheza Afrika
Mchezaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta anaechezea timu ya TP Mazembe ametajwa katika kinyanganyiro cha kugombea tuzo ya Mchezaji Bora Africa anayechezea Ligi za ndani.

CAF imetoa majina ya Tuzo mbili ile ya Mwanasoka Bora wa Mwaka Afrika na Mwanasoka Bora wa Mwaka Anayecheza Afrika ambayo Mbwana Samatta anatajwa kuwania.

Samatta ambaye pia ni mshindi wa Tuzo ya Mchezaji bora wa mwaka wa Goal kwa mwaka 2014 atagombea tuzo hio na wachezaji wengine 23 kutoka bara la Afrika wakimemo Robert Kidiaba na Roger Assalé anaocheza nao T.P Mazembe

2 comments: