Recent Posts

Xavi; Ningechezea Manchester united kama ningehamia ligi ya Epl

Chelsea, Manches United, City, Arsenal, Liverpool, hivi ni miongoni mwa vilabu vikubwa zaidi ulimwenguni na ni wachezaji wachache sana duniani ambao wasingependa kutundika daruga kabla ya kuvichezea..

  
Kiungo wa zamani wa FC Barcelona Xavi Hernandez amezungumzia namna ambavyo angependa kujiunga na moja ya vilabu hivyo kama ingebidi kuihama Barca wakati akiwa kwenye ubora wake.

  
Xavi anasema kama ingetoke kuhamia katika ligi kuu ya Uingereza basi angependa kujiunga na klabu ya Manchester United, kama alivyokaririwa na Eurosport.
. Kiungo huyo mwenye miaka 35 aliondoka FC Barcelona baada ya kuitumikia kwa miaka 17, na kwenda kumalizia soka huko alipo sasa katika klabu ya Al Sadd ya Qatar.

Xavi, ambaye ni mchezaji namba kwa kuichezea Spain mechi nyingi (mechi 133), anatajwa kuwa mmoja wa wanasoka bora kabisa kuwahi kutokea katika kizazi chake na alipokuwa kwenye ubora wake hakuna klabu kubwa yoyote iliyokuwa haitamani kuwa na mchezaji wa aina yake.

Alipoulizwa ni klabu gani ya Ligi kuu ya England angependa kuichezea, kiungo huyo akaitaja klabu yenye mafanikio zaidi katika EPL.
“Timu yenye historia, aidha Manchester United au Liverpool. Nafahamu timu nyingine kama Man City wameibuka hivi sasa, lakini Manchester United ndio chaguo langu zaidi.”

No comments