Recent Posts

Taifa Stars yasonga mbele, na sasa kuwavaa Algeria


Taifa Stars yasonga mbele, na sasa kuwavaa Algeria
Taifa Stars imefanikiwa kutinga katika hatua ya mwisho ya mchujo kuelekea kwenye hatua ya makundi ya kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia, licha ya kufungwa 1-0 na Malawi .
Tanzania inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 2-1, baada ya Jumatano kushinda 2-0 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa wa Angola, Martins de Carlvalho aliyesaidiwa na Gadzikwa Bongani wa Zimbabwe na Valdmiro Ntyamba wa Angola, hadi mapumziko Malawi walikua wanaongoza kwa bao 1-0, lilifungwa na John Banda dakika ya 42.
Kipa Ally Mustapha aliendelea kuwa shujaa kwa kuokoa michomo kadhaa katika mechi hio na kuendelea kuiweka Stars mchezoni. Barthez alifanya fanya kazi nzuri dakika ya 2 na ya 10 baada ya kuokoa michomo mfululizo ya Malawi.
Kutokana na ushindi huo, Stars inatarajia kucheza mechi mbili dhidi ya Algeria ambazo zitachezwa kati ya Novemba 9 na 17.
Kikosi cha Tanzania kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Shomary Kapombe, Mwinyi Hajji, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Himid Mao, Thomas Ulimwengu, Said Ndemla/John Bocco dk46, Mudathir Yahya, Mbwana Samatta na Farid Mussa/Mrisho Ngassa dk75.
Malawi; Simplex Nthala, Stanley Sanudi, Miracle Gabeya/Robin Ngalande dk76, Yamkani Fadya, Limbikani Mzava, Gerald Phiri, Chimango Kayira, Micium Mhone, Chiukepo Msowoya, John Banda na Shumaker Kuwali.

No comments