Recent Posts

VIDEO: Ufaransa wamepata ushindi mwingine wa Euro 2016 June 15 2016

Burudani ya michuano ya Euro 2016 bado inaendelea kama kawaida katika ardhi yaUfaransa, June 15 2016 ilichezwa michezo mitatu pamoja na mwenyeji wa michuano hiyoUfaransa alicheza dhidi ya Albania katika uwanja wa Stade Velodrome wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 60000.
Huo ulikuwa ni mchezo wa pili kwa timu hizo mbili za Kundi A na ulikuwa ni muhimu kwa timu zote mbili kupata matokeo ili kuweza kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele,Ufaransa ambao walikuwa nyumbani walifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-0, magoli ambayo yalifungwa na Antoine Griezman dakika ya 90 na Dimitri Payet katika dakika za nyongeza.
Kwa ushindi huo Ufaransa wanakuwa wamepata nafasi ya kutinga hatua inayofuata na wanasubiri kucheza mchezo wao wa kukamilisha ratiba wa Kundi A dhidi yaSwitzeland, ushindi huo umeifanya Ufaransaitimize jumla ya point sita na kuongoza msimamo wa Kundi A kwa tofauti ya point mbili dhidi ya Switzeland anayefuatia

ALL GOALS: UFARANSA 2-O ALBANIA



No comments