Recent Posts

Klabu kubwa ya Ulaya kuipiku Man United kwenye saini ya Zlatan Ibrahimovic


Mabingwa wa Bundesliga Bayern Munich wanataka kuipiku Manchester United kwenye saini ya mshambuliaji wa zamani wa PSG Zlatan Ibrahimovic, ripoti kutoka The People’s Person.

Taarifa nyingine zadai kwamba Manchester United imekamilisha dili na  Mswedi wa kimataifa, ambapo vipimo vya afya vyatarajiwa kufanywa baada ya michuano ya Euro 2016.

Lakini meneja mpya wa Bayern Carlo Ancelotti, aliyekuwa mkufunzi wake katika PSG, anataka kumleta mshambuliaji huyu katika Allianz Arena.

Anamhitaji kuchukua nafasi ya Robert Lewandowski ambaye anaweza kukamilisha uhamisho wake hivi punde kuelekea Real Madrid.

No comments