Recent Posts

Amissi Tambwe apania kufikisha mabao 25


KINARA wa mabao kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, Amissi Tambwe, amesema viwanja vya mikoani vitampa taji la mfungaji bora msimu huu na atafikisha mabao 25.

Yanga imebakisha mechi tatu kumaliza ligi na zote itacheza ugenini katika viwanja vya Nangwanda Sijaona, Mtwara, Sokoine, Mbeya na Majimaji Songea.

Tambwe amesema katika mechi hizo ana uhakika wa kufunga mabao matano na kufikisha mabao 25 na kubeba tuzo hiyo ya mfungaji bora.

Tambwe ambaye sasa ana mabao 20, alisema pamoja na ubovu wa viwanja vya mikoani, lakini yeye amekuwa akivijulia na kufunga mabao muhimu kwa timu yake, ambayo kwa sasa ipo nafasi nzuri ya kunyakua ubingwa msimu huu.

“Nina uzoefu mkubwa na viwanja vya mikoani kwa sababu uwanja ninaofanya mazoezi yangu binafsi ni mbaya kama vilivyo vya mikoani, ndiyo maana mimi huwa ninapocheza huko nafanya vizuri,” alisema Tambwe.

No comments