Beki wa Simba SC aelezea juu ya changamoto anazozipata nchini Ujerumani
Beki wa zamani wa Simba SC, Emily Mgeta ambaye anakipiga na timu ya Neckarsulmer Sport-Union ya nchini Ujerumani ameelezea changamoto kubwa anazokutana nazo nchini humo
Emily Mgeta.
Mgeta ameuambia mtandao wa Soka360 kwamba changamoto kubwa anayokutana nayo ni lugha kwa kuwa kila anayekwenda nchini humo lazima ajifunze lugha yao.
Emily Mgeta ameendelea kuelezea kusema kuwa changamoto nyingine ni ugeni na nchini humo kwa kuwa ndio mara yake ya kwanza kucheza mpira barani Ulaya, akiwa kama mchezaji mweusi pekee kikosini humo amesema inahitaji uvumilivu wa hali ya juu kutokana na magumu kadhaa anayoyapitia.
“Huku kwanza changamoto kubwa ni lugha maana ukija huku lazima ujifunze lugha yao, na pia ukiangalia mimi ndio kwanza naanza kucheza ligi Ulaya kwa maana Tanzania na huku tumepishana vitu vingi sana.
“Ukiangalia mimi ndio mtu mweusi pekee katika timu kwahiyo kuna muda nakuwa napata wakati mgumu lakini ndo hivyo yahitaji uvumilivu wa hali ya juu” alisema Mgeta.
Licha ya hali kuwa tofauti na Tanzania, mchezaji huyo aliyeibukia katika kikosi cha pili cha Simba SC, ameonyesha hali ya kupambana sanjari na kutokata tamaa huku akiendelea kupambana
Source; soka360.co.tz
No comments