Recent Posts

AC Milan kumpeleka mahakamani Yusupha Yaffa baada ya kudangaya umri ana miaka 19 wakati ana 28


Mshambuliji wa kiafrika na Gambia atuhumiwa kwa kosa la kudanganya umri nchini italia katika klabu ya Ac milan.
Kuna tatizo moja Yaffa anasema ana miaka 19 wakati ana miaka 28.
Kutokana na habari sasa Yaffa keshaitwa mahakamani kwa kosa hilo kwa ajili ya kusimewa mashitaka sasa.

Habari kuhusu umri wa ukweli wa Yaffa ulianza kujulikana kutokana na mitandao ya kijamii.
Ni baada ya rafiki yake waliyesoma nae kuandika umri wake kwenye akaunti yake ya facebook ndipo watu wakaanza kujiuliza

Kulingana na gazeti la italia Gazzetta dello sport,Yaffa anaeleza kuwa vyeti vyake vya kuzaliwa alivipoteza, na alipofika ofisi za uhamiaji nchini italia 2009 alisema kuwa alizaliwa tarehe 31 decemba 1996 badala ya tarehe 14 novemba 1987.

Hii sio mara ya kwanza Yaffa kujikuta kwenye vyombo vya sheria kwani mwezi January mwaka 2015 baada ya kuhamia frankfurt alituhumiwa kwa kubaka na kukamtwa.

Gazeti pia limeripoti kuwa wakati Yaffa akipinga kosa hilo mahakamani trainers pamoja na makocha wa milan watakuwepo pamoja na Filipo Inzaghi.

No comments