Recent Posts

WAPINZANI WA MAN UNITED WAANDAMWA NA MAJERUHI

Mechi mbili zinazofuata za Manchester United katika Ligi Kuu ya Uingereza ni dhidi ya Everton katika uwanja wa Goodison Park na Manchester City, Old Trafford.


Timu zote zinatarajiwa kuwa na majeruhi wengi ambao ni wachezaji muhimu katika vikosi vyao katika mechi zilizo mbele yao.

Everton

Manchester United watasafiri kwenda Everton Jumamosi hii kwa ajili ya mechi yao ya mchana. Everton watamkosa beki chaguo lao la kwanza Leighton Baines; beki wa kulia Tony Hibbert; kiungo wao mahiri Steven Pienaar na nyota wa zamani wa Manchester United Tom Cleverley.

Hata hivyo mabeki mawili chipukizi wa Everton Brendan Galloway na Tyias Browning wamecheza vizuri sana dhidi ya Swansea, West Brom na Liverpool.

Pamoja na yote, mastaa John Stones na Muhamed Bešić watakuwa na jukumu zito kuibeba timu yao dhidi ya Mashetani wekundu. Stones ni mchezaji muhimu katika safu ya ulinzi ya Everton licha ya kuwa na umri wa miaka 21.

 

Manchester City

Mahasimu hawa wakubwa wa United wana wachezaji wenye uwezo mkubwa sana katika kikosi chao, lakini wachezaji wao wa kikosi cha kwanza watakosekana katika safari yao kwenda Old Trafford Jumapili ya tarehe 15 Oktoba.

Mabeki wa kushoto Aleksandar Kolarov na Gaël Clichy ni majeruhi, Clichy pekee ndiye anayetarajiwa kurejea mapema kwa ajili ya mechi hiyo kubwa.

Samir Nasri na Yaya Touré wanasumbuliwa na majeraha ya misuli ya paja kwa sasa na wanaweza kurudi kazini wikiendi hii, lakini imeripotiwa kuwa majeraha ya Yaya yanaweza kumuweka nje kwa muda mrefu zaidi ya ilivyodhaniwa hapo awali.

Katika mapumziko ya kimataifa, Man City ilipoteza nyota wake wakubwa wanaoongea lugha ya Kihispaniola. David Silva anatarajiwa kuwa nje hadi mwezi ujao kutokana na majeraha ya kifundo cha mguu na kinara wa mabao Sergio Agüero anatarajiwa kuwa nje mpaka mwezi Novemba.
 

Orodha ya majeruhi wa Manchester United kwa sasa inaongozwa na Paddy McNair aluepasuka ini na Luke Shaw,  ambaye anauguza mguu wake uliovunjika.

Lakini pia viungo wa kati wa Manchester United wanasumbuliwa na majeraha ya muda mrefu. Bado yapo maswali kama wataweza kustahimili vishindo vya mechi dhidi ya Everton na CSK Mosco na bado wakawa fiti kwa mechi kubwa dhidi ya Manchester City

No comments