Recent Posts

Video: Obama amshauri Kanye West kuhusu kugombea urais 2020



Rais Barack Obama ametoa baadhi ya ushauri kuhusiana namna ya kufanya kama unataka kuwa rais wa Marekani baadae, huku akikisifia kidogo Chama cha Republic.
Lakini ungemtegea Obama kuwapa dondoo watu kama Hillary Clinton, Joe Biden au labda Donald Trump, Rais alikuwa hasa akimshauri Kanye West.
Rais wa Marekani Barack Obama
Rais wa Marekani Barack Obama
Wakati akizungumza katika uchangishaji fedha wa Kamati ya Taifa ya Democratic mjini San Francisco, Obama alijadili matarajio Kanye kuhusu kugombea urais kabla ya kupanda jukwaani na kuburudisha siku ya Jumamosi.
“Muda mchache utakwenda kumsikia mtu ambaye nasikia amekuwa akizungumza kuzindua kampeni za kuwa kiongozi wa siasa,” alisema Obama.
Kanye West akiwa na familia yake jijini San Francisco
Kanye West akiwa na mkewe Kim Kardashian jijini San Francisco
Obama alitania: “Unaweza kusikia hilo. Kanye anafikiria kugombea kuwa Spika wa Bunge.”
Kanye, ambaye anasema atagombea kuingia Oval Office mwaka 2020, alipewa onyo kwamba anapaswa kufuata sheria tatu muhimu kama anataka kuwa rais wa Marekani.
Barack Obama akiwa na Kanye West na Kim KardashianBarack Obama akiwa na Kanye West na Kim Kardashia

No comments