TFF NHIF WASAINI MKATABA
Katibu
Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Mwesigwa Selestine
leo amesaini mkataba wa mwaka mmoja na mfuko wa huduma ya afya (NHIF)
kwa ajili ya kutoa huduma kwa wachezaji wa Ligi Kuu pamoja na viongozi
wa benchi la ufundi
.
Hafla ya kusaini mkataba huo
imefanyika katika hoteli ya Protea Courtyard iliyopo Upanga jijini Dar
es salaam ambapo katibu mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine na Mkurugenzi wa
Masoko na Utafiti wa NHIF Rehani Athumani walisaini kwa niaba ya pande
hizo mbili.
Akiongea na waandishi wa habari
wakati wa mkutano wa uwekaji sahihi mkataba huo, Mwesigwa amesema
anaishukuru NHIF kwa kudhamini kutoa huduma ya afya kwa wachezaji na
mabenchi ya ufundi kwa vilabu vyote 16 vinavyoshiriki Ligi kuu ya
Vodacom.
Aidha Mwesigwa ameviomba vilabu
vya Ligi Kuu nchini kutoa ushirikiano na watoa huduma ya afya kwa
wachezaji na viongozi kutoka NHIF pindi watakapokuwa wanafika kwenye
vilabu vyao kwa ajili ya shughuli mbalimbali.
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti
wa NHIF, Rehani Athumani akiongea kwa niaba ya mfuko huo amesema wako
tayari kufanya kazi na kutoa huduma ya afya kwa ngazi zote ikiwemo kwa
timu za madaraja ya chini pia.
TFF na NHIF zimeingia mkataba wa
mwaka mmoja wa udhamini wa huduma ya afya kwa wachezaji wa ligi kuu na
viongozi wa benchi la ufundi, mkataba ambao unaeza kuongezwa kila
unapomalizika.
TFF kwa kupitia bodi ya ligi
inavitaka vilabu vyote vya Ligi Kuu vitoe ushirikiano kwa wafanyakazi wa
NHIF katika kurahisiha shughuli za usajili ikiwa ni pamoja na kutoa
taarifa na nyaraka sahihi zikiwemo picha za wahusika katika muda sahihi.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF
No comments