Recent Posts

SIMBA HAWANA MASIHARA WAMESHAFIKA MBEYA KUSAKA POINT TATU

Timu ya Simba SC ‘Mnyama’ tayari imeshawasili jijini Mbeya kwa ajili ya kuikabili timu ya Mbeya City kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara unaotarajiwa kupigwa mwishoni mwa juma hili katika dimba la kumbukumbu ya Sokoine, jijini Mbeya.

Afisa habari wa wekundu wa Msimbazi Haji Manara amethibitisha kikosi chao kuwasili salama mkoni Mbeya na kimeanza maandalizi ya mchezo dhidi ya Mbeya City na baadae kitamenyana na timu ya Tanzania Prisons kwenye uwanja huohuo wa Sokoine.

“Tuko Mbeaya na timu inaendelea na mazoezi, kunatofauti kubwa ya hali ya hewa kati ya Dar es Salaam na Mbeya kwahiyo waataalamu wanasema ni vizuri ukawahi kufika au ukafika siku moja kabla ya mechi, ndivyo tunavyoambiwa na wataalamu wa hali ya hewa”, amesema Manara.

“Tumefika mapema ili wachezaji wasiathirike na hali ya hewa ya Mbeya, tunafanya mazoezi kujiandaa na hizi mechi mbili za Mbeya City na Prisons. Tuko hapa kwa ajili ya kutafuta pointi sita hakuna namna nyingine”.

“Wachezaji wetu ambao walikuwa kwenye timu ya taifa bila shaka leo wataingia Mbeya kujiunga na wenzao baada ya kuwasili jana jijini Dar es Salaam wakitokea Malawi. Tunamajeruhi mmoja Emery Nimubona lakini wachezaji wengine wote wako sawa”

No comments