Recent Posts

Manchester united: De gea amtaja Chicharito kama mshambuliaji bora Trafford


Kipa wa man utd David De Gea amemtaja Chicharito kama mshambuliaji bora kuliko Wyne Rooney, Robin van Persie na Radmel Falcao.

Chicharito aliuzwa Bayern Leverkusen kipindi cha dirisha la usajili baada ya kutoka Real Madrid alipokuwa anacheza kwa mkopo.

Lakini De Gea amemtaja mmexico huyo kama mshambuliaji bora kuliko Wyne Rooney na washambuliaji wengine wa Man utd.

Aliulizwa yupi ni mshambuliaji bora ambae umecheza nae tokea umekuja old trafford kupitia website ya man utd, De Gea akajibu: "Rafiki yangu Chicharito."

Hernandez,27, amefunga magoli mawili kwenye mechi saba alizocheza tokea ajiunge na leverkusen kwa kiasi cha £7m kipindi cha dirisha la usajili.

Chicharito amefunga magoli 59 kwenye mechi 157 za man utd tokea ajiunge akitokea Guadalajara 2010.

No comments