Recent Posts

REKODI STAAJABU 10 ALIZOWEKA CRISTIAN RONALDO KWENYE SOKA DUNIANI

Rekodi 10 STAAJABU Duniani zilizoandikwa na Cristiano Ronaldo
Staa wa Real Madrid Cristiano Ronaldo huonekana kama mmoja wa wachezaji
bora katika historia ya soka duniani baada ya kuwa mchezaji wa kwanza kushinda tuzo la FIFA Ballon d'Or katika timu mbili tofauti, mwaka 2008 (Manchester United), 2013 na 2014 (Real Madrid), na pia alivunja rekodi nyingi katika ulimwengu wa soka.
Alianza shughuli yake ya soka katika klabu ya Ureno Sporting Lisbon kabla ajiunge na Manchester United mnamo 2003, ambapo alipata mashabiki wengi ulimwenguni kote.
Hebu, tuangalie rekodi 10 staajabu Ronaldo alizoandika hadi sasa.
10. Mabao zaidi ya 40 katika misimu miwili mfululizo
Mreno wa kimataifa alikuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao 40 ya ligi katika misimu miwili mfululizo ambapo alivifanya kwa Real Madrid mnamo 2010-11 na katika kampeni ya 2011-12 alipofunga mabao 46.
9. Mchezaji wa kwanza kufunga bao katika kila dakika ya mchezo
Cristiano Ronaldo aliandika rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza anayeweza kufunga bao katika kila dakika ya mchezo; alitimiza rekodi hiyo alipofunga bao kunako dakika ya saba katika ushindi wa Real Madrid 2-0 dhidi ya wapinzani Atletico Madrid mnamo Februari 2013.
Lakini baadaye mwezi Septemba 2014, Zlatan Ibrahimovic naye alijiunga na Ronaldo kwenye orodha hiyo ya wachezaji wawili duniani wenye uwezo wa kufunga bao katika kila dakika ya mchezo.
8. Mchezaji pekee aliyeshinda kila kitu katika klabu mbili tofauti
Ronaldo ni mchezaji pekee aliyewahi kushinda kombe la ligi,  Domestic Cup, League Supercup, tuzo la mchezaji bora wa mwaka, Golden Boot, Ballon d’Or, Ligi ya Mabingwa na Kombe la Dunia la Vilabukatika klabu mbili tofauti (Manchester United na Real Madrid).
7. Mchezaji pekee katika historia kufunga mabao 60 mara nne mfululizo katika mwaka
Mshindi wa Ballon d’Or mara tatu aliweka rekodi ya kuwa mchezaji pekee katika historia aliyefunga mabao 60 au zaidi katika kalenda ya mwaka mara nne mfululizo tangu 2011 hadi 2014.
6. Kutajwa katika timu ya FIFA ya mwaka
Mreno wa kimataifa anamiliki rekodi ya kuonekana katika timu ya mwaka ya FIFPro World XI: mara 8 (2007-2014).
5. Mchezaji pekee aliyetajwa katikatimu ya FIFPro World XI kwa klabu mbili tofauti
Mchezaji pekee na wa kwanza kujitokeza katika FIFPro World XI kwa klabu mbili tofauti (Manchester United na Real Madrid).
4. Mchezaji pekee kufunga mabao zaidi ya 50 katika misimu 5 mfululizo
Staa wa Real Madrid Cristiano Ronaldo aliweka pia rekodi nyingine msimu uliopita ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao 50 katika misimu 5mfululizo.
2010-11: mabao 53
2011-12: mabao 60
2012-13: mabao 55
2013-14: mabao 51
2014-15: mabao 61
3. Mchezaji wa kwanza aliyekuwa mfungaji bora Ulaya katika ligi mbili
Ronaldo ni mchezaji pekee na wa kwanza kushinda “European Golden Shoe” katika ligi mbili (Ligi Kuu ya England akiwa Manchester United na La Liga akiwa Real Madrid).
 2. Mchezaji aliyefunga mabao mengi katika msimu mmoja wa Ligi ya Mabingwa
Ronaldo ni mmiliki wa rekodi ya kufunga mabao mengi katika msimu mmoja wa Ligi ya Mabingwa, ambapo alifunga mabao 17 katika msimu wa 2013-14.
1. Mchezaji pekee na wa kwanza kushinda ‘European Golden Shoe’ mara nne
Cristiano Ronaldo alipewa tuzo la “European Golden Shoe” mnamo miaka 2008, 2011, 2014 na 2015, na ni mchezaji pekee katika historia aliyeshinda “European Golden Shoe” mara nne.

No comments