Recent Posts

PAUL SCHOLES : PERFOMANCE YA MARTIAL NI PRESSURE KWA ROONEY


Paul Scholes anapata jina kubwa na kujijengea heshima kwenye swala la uchambuzi, hivi sasa amemgeukia Wayne Rooney. Kama wewe ni shabiki wa Wayne Rooney naomba ukumbuke kwamba Scholes aliwai kumsifia Kun Aguero kwamba ndie mchezaji pekee wa EPL anaeweza kucheza kwenye ligi yoyote ulaya na kufanya vizuri. Siku chache baada ya hapo Kun akatupia goli 5. Pia alisema ligi ya EPL haina world class player, wachezaji wa kiwango cha dunia wapo hispania, ujerumani na italy na tukashuhudia jinsi club kubwa za EPL zikipata shida kwenye UEFA kabla ya Arsenal kuwafutia aibu vigogo wenzake.

Sasa akiwa kwenye uchambuzi wa kituo cha BT Sport Scholes alisema,“Martia ni bado mdogo sana, ana miaka 19 na hakuja Manchester akiwa na jina kubwa kwenye kufunga magoli, lakini nadhani uwezo wake uwanjani unarudisha pressure kwa Wayne Rooney. Wakati sisi tupo Manchester tulikua na strikers 4 ambao wanaweza kufunga magoli 25 hadi 30 lakini kwa sasa timu haifanyi hivyo. Hii ni pressure kubwa kwa Rooney.”

Pia aliendelea kumsifia Martial kwa kusema,“Martial hakukata tamaa baada ya kitendo cha penati kutokea na baadae alifunga goli zuri. Ilitakiwa wa-push kila waliwezalo ili kupata goli la pili”

No comments