MSHAMBULIAJI WA CHELSEA DIEGO COSTA ATEMWA TIMU YA TAIFA HISPANIA
michezo miwili ya wiki ijayo, huku kocha Vicent Del Bosque akisema hajafurahishwa na tabia ya mchezaji huyo aliyoifanya dhidi ya Arsenal.
Costa ambaye ana goli moja tu katika michezo tisa aliyoichezea timu ya taifa ya Hispania anatumikia adhabu ya kadi za njano na alitarajiwa kuukosa mchezo dhidi ya Luxembourg lakini angeweza kupangwa dhidi ya Ukraine.
Spain inahitaji point moja tu kufuzu katika michuano ya mataifa ya Ulaya na wiki ijayo itambana na Luxembourg na Ukraine katika michezo yake ya mwisho ya kundi.
Mshambuliaji wa Juventus aliye katika fomu hivi sasa, Alvaro Morata ameitwa kikosini na anatarajiwa kumbadili Diego Costa katika kikosi cha kwanza.
Wachezaji wenza watatu wa Chelsea Cesar Azzpilicueta, Cesc Fabregas na Pedro Rodriguez wote wameitwa sambamba na Carzola wa Arsenal na wachezaji wawili wa Manchester United David De Gea na Juan Mata huku David Silva wa Manchester City akikamilisha orodha ya wachezaji 23.
Alipoulizwa kama tabia ya Costa katika mechi dhidi ya Arsenal imechangia kuachwa, Del Bosque alisema, “Hapana. Ila sikufurahishwa na tabia zake
No comments