Recent Posts

MESSI KWENDA JELA MIEZI 22

Masaa 24 tangu ilipotoka taarifa kwamba mwanasoka wa FC Barcelona
na Argentina Lionel Messi sasa atafunguliwa rasmi mashtaka mahakamani kwa kesi ya kukwepa kodi nchini Hispania – sasa tuangalie ikiwa atakutwa na hatia adhabu atakayopata.
 Ikiwa mwanasoka huyo atakutwa na hatia, adhabu ya kifungo cha miezi 22 itamkuta. Mwendesha mashtaka wiki iliyopita alisema Messi hana kesi juu ya ukwepaji kodi kutokana kwamba hakuwa na ufahamu wowote wa vitendo vya baba yake vya kukwepa kodi ya kinachofikia £3.5m kati ya mwaka 2007 na 2009.
Lakini jana Jaji wa mahakama alikubali ushauri wa mwanasheria wa serikali, ambaye alisema Messi inabidi asimame kizimbani kwa makosa matatu ya ukwepaji kodi. 
Adhabu ya juu kabisa ya kesi hii ni kifungo cha miezi 22.5 jela. 

No comments