Maguli aunganisha nguvu na Tambwe kuwachamba Simba
“Simba kama walivyofanya kwa Tambwe ndivyo hivyo walivyofanya kwa Elius Maguli dakika za mwisho za kuanza ligi hii msimu huu.”
Msimu wa ligi kuu 2013/14 Amisi Tambwe raia toka Burundi alitamba vilivyo na kikosi cha wanamsimbazi.
Mshambuliaji huyo aliibuka kinara wa kupachika mabao kwenye kikosi hicho lakini ujio wa Emanuel Okwi ulimfanya mchezaji huyo kuanza kuonekana si lolote si chochote.
Simba walianza kujiaminisha kiwango cha mrundi huyo kimeshuka. Yanga ilimtizama mrundi huyo kwa jicho la ufundi na kumvisha uzi wa kijani na njano.
Msimu wa 2014/15 Tambwe akiwa na Yanga alidhihirisha upofu wa Simba hao wa Kariakoo juu ya kipaji cha mshambuliaji huyo.
Tambwe katika msimu huyo amesimama kama mfungaji namba mbili ndani ya ligi kuu akicheza vizuri sana. Tambwe aliyepakwa matope ya kejeli kuwa ni ‘mviziaji tu’ anaonekana si tu kuwa mfungaji bali anahusika pia kwenye upishi wa mabao.
Uzuri wa mrundi huyo ulianza kuwasuta Simba na sasa wamekubali walikosea lakini hilo likiwa bado halijapoa, ukitazama msimamo wa wafungaji wa ligi kuu baada ya mechi zao utaliona jina la Elius Maguli likiwa kileleni na mabao 6.
Simba kama walivyofanya kwa Tambwe ndivyo hivyo walivyofanya kwa Elius Maguli dakika za mwisho za kuanza ligi hii msimu huu.
Elius Maguli iliaminika amekwisha na kuwaleta Hassan Mgosi na Pape Abdoulaye N’daw ambao mpaka hata hawana hata bao la kuotea.
Stand United wamefanya kama walivyofanya Yanga na sasa Maguli ni kinara kwenye kutupia ndani ya timu hiyo na ligi kuu
No comments