Recent Posts

Magazeti ya nchini Uingereza leo Octoba 20 habari za michezo yameandika haya


Danny Ings ambaye alifanyiwa upasuaji siku ya Jumanne kutokana na majeruhi aliyopata anaamini kuwa ataweza kurudi uwanjani kuitumikia Liverpool kabla msimu huu haujaisha.

Mshambuliaji wa Colombia Radmel Falcao ataachana na Chelsea mwezi January kama ataendelea kutokuwa na wakati mzuri Stamford Bridge.

Mchezaji wa zamani wa Liverpool Jonh Arne Riise amesema Daniel Sturridge anahitaji kuongeza uwezo zaidi kama anataka kuwa mshambuliaji chaguo la kwanza kwa kocha mpya Jurgen Klopp.

Jose Mourinho amesema:" Nipo katika moja ya msimu mbovu. Kuna watu wengine huwa wana msimu mmoja mzuri kati ya misimu 20. Na ameingeza kuwa hana marafiki wengi kwenye soka ulimwenguni".

Kocha Ronald Koeman amesema kuwa atakuwa na furaha kusaini mkataba mpya Southampton. Mkataba wake wa sasa unaisha msimu wa kiangazi 2017.

Bibi yake Radmel Falcao anailamu Manchester united na kocha wa chelsea kwa kuharibu uwezo wa kujiamini wa mshambuliaji huyo.

Kocha mpya wa Sunderland Sam Allardyce ameiyambia timu yake kuwa mchezo wao wa jumapili ndio waweza kuwaweka sehemu nzuri au kuwaharibia msimu  huu

Joe Cole anaamini kocha Tim Sherwood ataijenga Aston Villa kwa kutumia vijana wadogo.

No comments