Recent Posts

Ligi daraja la kwanza kuanza Novemba 14

Ligi ya Daraja la Pili kuanza Nov 14

Ligi Daraja la kwanza nchini (SDL) sasa itaanza Novemba 14 badala ya Oktoba 31 ili kutoa fursa kwa bodi ya Ligi kukamilisha maandalizi mengine ikiwemo viwanja vitakavyotumika kwa ajili ya michezo ya ligi hiyo.

Makundi ya FDL ni kama ifuatavyo; Kundi A ni African Lyon FC (Dar es Salaam), Ashanti United SC (Dar es Salaam), Friends Rangers FC (Dar es Salaam), Kiluvya United FC (Pwani), Kinondoni Municipal Council FC (Dar es Salaam), Mji Mkuu FC (Dodoma), Polisi Dar es Salaam FC na Polisi Dodoma FC.

Kundi B ni Burkina Faso FC (Morogoro), Kimondo SC (Mbeya), Kurugenzi Mufindi (Iringa), Lipuli SC (Iringa), Njombe Mji SC (Njombe), Polisi Morogoro FC na Ruvu Shooting FC (Pwani) wakati kundi C ni Geita Gold SC (Geita), JKT Kanembwa FC (Kigoma), JKT Oljoro FC (Arusha), Mbao FC (Mwanza), Panone FC (Kilimanjaro), Polisi Mara FC, Polisi Tabora FC na Rhino Rangers FC (Tabora).

No comments