Recent Posts

Kuelekea mechi dhidi ya Simba October 17, Mbeya City imeendelea na mazoezi bila kocha mkuu (+Pichaz)

Klabu ya Mbeya City ya jijini Mbeya ambayo  October 17 itaikaribisha Simbakatika uwanja wa Sokoine Mbeyakucheza mechi yake ya sita ya Ligi KuuTanzania bara msimu wa 2015/2016.Mbeya City ambayo inashika nafasi ya 13 baada ya kucheza mechi sita na kushinda moja na kutoka sare moja inashuka uwanjani kucheza ikiwa na huzuni.

Mbeya City kwa siku za hivi karibuni imeondokewa na aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo Juma Mwambusi ambaye ameenda kuwa kocha msaidizi wa klabu ya Yanga na kurithi mikoba ya Charles Boniface Mkwasa aliyepata mkataba wa kuwa kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars.

Kwa sasa Mbeya City ina mkosa kocha wake mkuu na nahodha wa klabu hiyoJuma Nyosso ambaye anatumikia adhabu ya kufungiwa kwa kipindi cha miaka miwili, lakini kwa sasa wanafundishwa na kocha wao msaidiziMeja Abdul Mingange bila kuwa na kocha mkuu. Hata hivyo Mbeya City imeendelea na mazoezi ya kuelekea mchezo huo ikiwa na nyota wake kama Juma Kasejana Haruna Moshi Boban.

Boban na Kaseja

No comments