Recent Posts

Haya ndio maamuzi ya Simba sc kuhusu kocha wao


Baada ya taarifa kuzagaa kwenye baadhi ya vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii kwamba kocha mkuu wa ‘wekundu wa Msimbazi’ Simba amekalia ‘kuti kavu’ kunako klabu hiyo kutokana na kufungwa mechi mbili kati ya saba, uongozi wa klabu hiyo umeibuka na kukanusha taarifa hiyo kuwa si ya kweli.

Taarifa zilienda mbali zaidi na kudai kuwa, kocha huyo amepewa mechi moja (dhidi ya Coastal Union) na endapo atapotea mchezo huo basi huenda mkataba wake na klabu hiyo ukasitishwa.

Afisa habari wa klabu ya Simba Haji Manara amesema taarifa hizo si za kweli na kuongeza kuwa, bado ni mapema kufikia uamuzi kama huo kwasababu bado kuna mechi nyingi na mpaka sasahivi bado bingwa hajulikani huku kila timu inayoshiriki ligi hiyo bado ina nafasi ya kuwa bingwa.

“Tunawaomba wapenzi wa Simba watulie mambo mazuri yanakuja, uamuzi utafanywa wa busara kwa mustakabali wa klabu ya Simba pale itakapobidi. Lakini kawa sasa tuko vizuri hatuna mpango wa kutimua kocha yeyote tuna endelea na mikakati yetu”, amesema Manara.

Simba ilipoteza mechi yake ya raundi ya saba ilipokubali kulala mbele ya Tanzania Prisons kwa goli 1-0 kwenye uwanja wa Sokoine, Mbeya. Awali Simba ilipoteza mchezo wake wa kwanza msimu huu dhidi ya Yanga kwa kufungwa kwa goli 2-0 kwenye uwanja wa taifa.

No comments