Recent Posts

HAWA NDIO WABABE WA RONALDO KWENYE UPANDE WA KUTUPIA MAGOLI NYAVUNI


Wiki hii Ronaldo amezungumziwa sana baada ya kufikisha magoli 500, basi hawa hapa ndio baba zake
na kwenye kufumania nyavu. Magoli haya ni kutoka kwenye official match tu.
10) James McGrory alicheza kati ya 1922 hadi 1937, huyu jamaa ni raia wa Scotland na alitupia magoli 550.
9)Eusebio huyu ni legend wa Ureno na katika maisha yake ya soka alitupia nyavuni mara 552. Amecheza soka kati ya miaka 1957-1979
8)Ernst Willimowski amefunga magoli 554 na amecheza soka kwenye miaka ya 1934-1995. Huyu jamaa ni rais wa Ujerumani
7)Uwe Seeler ametupia nyavuni mara 575 na amecheza soka kwenye miaka ya 1954 hadi 1978. Huyu pia ni raia wa Ujerumani.
6)Ferenc Deak alifunga magoli 576 katika miaka yake ya kucheza soka ambayo ni 1944 hadi 1954. Huyu ni raia wa Hungury
5)Gerd Muller huyu ni mjerumani ambae kwenye maisha yake ya soka ameshawai kutupia mara 735
4)Ferenc Puskas huyu mbabe wa kutupia ameshafunga magoli 746 na amecheza kati ya miaka 1943 hadi 1966. Raia wa nchi ya Hungury
3) Pele ametupia magoli 767 kwenye official mechi achana na ambazo hazikua official. Rais huyu wa Brazil amecheza kati ya miaka ya 1956 hadi 1977
2)Romanario amecheza soka kati ya miaka ya 1985 hadi 2009 na alifunga magoli 772.
1)Josef Bican ndio baba yao kwenye kufumania nyavu ametupia mara 805. Huyu alikua ni raia wa Czech-Austrian

No comments