Recent Posts

Djibril Cisse afunguliwa mashtaka kisa kuvujisha mkanda wa ngono

Mshambuliaji wa zamani wa klabu yaLiverpool ya Uingereza na timu ya taifa yaUfaransa Djibril Cisse ameingia kwenye headlines asubuhi ya October 13 baada ya kukamatwa kwa kosa la kuvujisha mkanda wa ngono. Djibril Cisse ni moja kati ya watu waliokamatwa Jumanne ya October 13 Versailles Ufaransa.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa vilabu vya LiverpoolAuxerreMarseille,Sunderland, Lazio na Panathinaikosameingia katika tuhuma hiyo akiwa pamoja na mchezaji mwenzake wa zamani Mathieu Valbuena ambao wamewahi kucheza pamoja.

Djibril Cisse na Mathieu Valbuena

Djibril Cisse ambaye amewahi kutwaa kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2005 akiwa na klabu yake ya zamani yaLiverpool, amewahi kulalamika polisi kumfuatilia na kumchunguza kufuatia tuhuma hizo mwaka 2008. Djibril Cisseambaye ana umri wa miaka 34 kwa sasa hana timu ya kucheza. Kesi dhidi ya tuhuma hizo bado inaendelea kufanyiwa uchunguzi ila hizi ni taarifa za awali.

No comments