Recent Posts

Diego Simeone kuchukua nafasi ya Jose Mourinho chelsea.


Mmiliki wa klabu ya chelsea Roman Abromovich ana mpango wa kumpa kibarua kocha wa Atletico madrid Diego Simeone ili achukue nafasi ya Jose Mourinho ambae anataka kumfukuza, habari kutoka gazeti la independent Uingereza.
Kocha huyu mreno kwa sasa yupo katika mbali mbaya ndani ya Stamford bridge baada ya kuanza vibaya msimu wa ligi ambapo chelsea inashika nafasi ya 16

Kama kocha huyo mwenye miaka 52 ataachishwa kazi yake Stamford bridge kocha anaetegemewa kuja kuchukua nafasi hiyo ni kocha wa Atletico madrid Diego Simeone.

Diego simeone mwenye miaka 45 ameiwezesha Atletico madrid kutwaa kombe la ligi ya Hispania na kucheza fainali ya klabu bngwa Ulaya kwenye msimu mmoja miezi 18 iliyopita. Kocha huyo Muargentina alisaini mkataba wa kubaki Vicente Carderon kwa ada ya £15 milioni.

Chelsea mechi inayofuata watacheza dhidi ya Aston villa Jumamosi Stamford bridge.

Ikiwa chelsea watapoteza mechi hii ya Jumamosi ndio utakawa mwisho wa kocha huyo anaejiita special one.


No comments