Recent Posts

ANDREY COUNTINHO:SIWEZI KUHAMIA SIMBA

 Andrew Coutinho (L) of Yanga FC contest for ball with Ibrahim Warsama of Telecom FC

Coutinho aliyetua Yanga msimu uliopita akisajiliwa na kocha Marcio Maximo
KIUNGO wa kimataifa wa Yanga raia wa Brazili Andrey Coutinho, amesema hana mpango wa kuihama timu hiyo licha ya kukosa namba kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Mholanzi Hans van der Pluijm.
Coutinho aliyetua Yanga msimu uliopita akisajiliwa na kocha Marcio Maximo, amesema yupo tayari kumaliza miezi saba ya mkataba wake huku akipigania nafasi ya kucheza kwenye timu hiyo kuliko kujiunga na wapinzani wao Simba ambapo kufanya hivyo ni sawa na kuisaliti klabu hiyo iliyomleta Tanzania.
“Japokuwa soka ndiyo kazi yangu lakini niseme ukweli siwezi kuhamia Simba naiheshimu Yanga kwasababu ndiyo klabu ambayo imenifanya niijue Tanzania na nimepata ubingwa nikiwa hapa kitu chamsingi kwangu ni kuhakikisha napigania namba kwenye kikosi cha kwanza hadi hapo mwihoni mwa msimu,”amesema Coutinho.
Tangu kuanza msimu huu katika mechi tano ambazo Yanga imecheza Coutinho, amecheza mechi moja dhidi ya Mtibwa Sugar, iliyochezwa uwanja wa Jamhuri Morogoro ambapo Yanga ilishinda kwa mabao 2-0 na yeye aliingia akitokea benchi kuchukua nafasi ya Simoan Msuva dakika ya 75.

No comments