WACHEZAJI WA TANZANIA WANAOTARAJIWA KUTIMKIA NJE YA NCHI MSIMU UJAO
Kuna tetesi kibao za wachezaji kuhama klabu zao Ligi Kuu Bara dirisha la uhamisho litakapofunguliwa, wengine wanatarajiwa kwenda nje ya nchi kabisa, ni akina nani?
Endelea kusoma upate kujua ni wachezaji gani klabu zao zinaweza kuwauza nje ya nchi kushiriki ligi mbalimbali ndani na nje ya Afrika, ligi tofauti na Ligi ya Vodacom Tanzania Bara.
Farid Mussa | Azam FC
Tayari kuna habari kuwa ameshafuzu majaribio katika klabu ya daraja la pili Tenerrife, kinachosubiriwa ni makubaliano kati ya Azam Fc na Tenerrife kuhusu ada ya uhamisho wa winga huyo, na Azam wapo tayari kumruhusu hata kwa mkopo ili akacheze soka Hispania kwa msimu ujao, anatazamiwa kukosekana kwenye kikosi cha Azam kwa msimu ujao.
Ibrahim Ajib | Simba SC
Kupitia kwa wakala wake bwana Juma Ndambile anathibitisha Ajib amefuzu kwa majaribio katika klabu ya Golden Arrows ya Afrika Kusini, na mazungumzo yameshaanza kati ya Simba na mchezaji husika kuhusu kuondoka kwenda kucheza Afrika kusini kwa msimu ujao.
Elias Maguri | Stand United
Aliingia kwenye mgogoro na mkufunzi wake wa Stand united Patric Leiwing baada ya kwenda kufanya majaribio katika klabu ya Al ahly ya Misri, licha ya kutufanya vizuri kwenye majaribio hayo inasemekana tayari amepata timu nyingine nchini Oman na anatarajiwa kucheza huko msimu ujao.
Kelvin Friday | Azam FC
Winga wa Azam aliye kwa mkopo kwenye klabu ya Mtibwa, anatazamiwa kujiunga na St George ya Ethiopia baada ya dili lake kushindikana msimu uliopita, Azam wako tayari kufanikisha dili hilo ili mchezaji aweze cheza katika ligi kuu ya Ethiopia kwa msimu ujao.
No comments